Timu ya Azam imepoteza ushindi kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 na Ruvu Shooting katika uwanja wa Chamanzi jana.
Azam imepata pointi 1 pekee katika michezo 3 ya mwisho ambayo timu hiyo imecheza hadi sasa, imepoteza mechi mbili dhidi ya Simba na Ndanda ya Mtwara na jana ilishindwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kugawana pointi na Ruvu Shooting.
Mechi ilikuwa ni kama yenye kubadilishana matokeo ambapo Ruvu Shooting ilipata bao Maganga na Jean Mugiraneza alichomoa bao hilo kabla ya kipindi cha mapumziko.
Hali ilikuwa hivyo kipindi cha pili ambapo Azam ilianza kupata bao la pili kupitia Hamis Mcha aliyefunga dakika ya 70 lakini hata hivyo Shaban Kisiga 'Maloney' alichomoa bao hilo kabla ya kumalizika kwa mpira.

Comments
Post a Comment