Timu ya Azam leo katika uwanja wa Chamanzi itaikribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu utakaochezwa majira ya saa 1 za usiku.
Azam haijapata ushindi katika mechi tano za mwisho na leo inaingia kwenye kibarua kingine cha kuwakabili wababe hao wa Manungu kutoka mkoani Morogoro.
Hadi sasa Azam inakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 12 ikiwa imeachwa kwa pointi 3 na Yanga yenye mchezo mkononi na pointi 11 nyuma ya Simba yenye pointi 23.

Comments
Post a Comment