Baada ya Hans Pluijm kujiuzulu kuinoa timu ya Yanga zipo tetesi huenda kocha huyo akatua Azam ambao wameanza mazungumzo nae kwa siri.
Pluijm alilazimika kuiandikia Yanga Barua ya kujiuzulu kutokana na timu kuanza mazungumzo na kocha mpya Mzambia George Lwandamina ambaye ameshasaini miaka miwili kuwanoa wana jangwani hao.
Azam bado haijawa na mwenendo mzuri kwenye ligi tangu alipotua mhispania Zeben Hernandez kuwanoa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati.
Pia inasadikia huenda Azam ikandaa mpango wa kumfanya Pluijm kuwa kocha wa mkuu wa timu hiyo au mkurugezi wa benchi la ufundi.

Comments
Post a Comment