Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania maarufu kama Serengeti Boys wanatarijiwa kuwasili leo wakitokea Congo Brazzaville baada ya mchezo wa marudiano.
Serengeti Boys ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-2 nyumbani ilishindwa kutetea ushindi wake baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mechi yao.
Endapo Serengeti boys wangepata hata sare kwenye mechi wangekuwa wamejikatia tiketi ya kufuzu kwenye fainali za kombe la mataifa Afrika kwa vijana (U 17) ambazo zitafanyika nchini Madagascar.

Comments
Post a Comment