Wataalamu wa ufundi wa Shirikisho la Mpira barani Afrika (CAF) huenda wakatua nchini muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya ukaguzi wa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Huu ni utaratibu wa CAF ambao baada ya muda hutembelea nchi au wanachama kuangalia maeneo ya miundo mbinu ya mpira kabla ya kupandisha hadhi ya viwanja kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayoendeshwa na CECAFA, CAF au FIFA.
Hadi sasa ni viwanja vinne ambavyo vinatambuliwa na FIFA nchini Tanzania ukiwemo uwanja wa Amani Zanzibar, Kaitaba Kagera, Azam Complex na uwanja wa Taifa.
Uwanja huo utaungana na kiwanja cha Gombani Pemba, Sokoine Mbeya na Kaitaba wa Kagera ambayo ambavyo vimeshakaguliwa na huenda vikatumika kimataifa baada ya majibu kutolewa.

Comments
Post a Comment