Licha ya kushinda mechi iliyopita dhidi ya Mbao FC ya Mwanza timu ya Majimaji imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar.
Kagera Sugar imepoza machungu ambapo wiki iliyopita ilipoteza mechi baada ya kukubali kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Toto Africans katika uwanja wa kaitaba.
Matokeo hayo yanazidi kuiweka pabaya timu hiyo ikiwa ni pamoja na kumpa kibarua kizito kocha wa sasa Kally Ongala ambaye ameichukua timu hiyo siku za hivi karibu.

Comments
Post a Comment