Blagnon: VPL si mchezo


Mshambuliaji wa timu ya Simba Fredrick Blagnon amesema kuwa ligi ya Tanzania ni ngumu kinyume na matarajio yake wakati akisajiliwa na Simba.

Blagnon amefunga bao moja tangu alipotua Simba katika mechi ya kwanza dhidi ya Ndanda ya Mtwara zikiwa zimechezwa mechi 9 mpaka kwenye ligi kuu.

"Mwanzoni nilidhani nitainjoi nikicheza mpira Tanzania, lakini mambo magumu unahjitaji kupambana ili kuipa timu mafanikio na kujipa mafanikio binafsi."

"Hakuna kazi kwenye kila ligi na ndivyo ilivyo Tanzania mambo ni magumu sikuwahi kufikiria aina hii ya upinzani." Alisema Blagnon.

Pamoja na Kocha Joseph Omog kumpa Blagnon nafasi ya kuanza kwenye mechi mbili zilizopita lakini mchezaji huyo ameshindwa kutumia nafasi hiyo kufunga magoli.

Comments