Bruce achukua Mikoba ya Di Matteo Villa Park


Baada ya kuondolewa kwa Aliyekuwa kocha wa Aston Villa Roberto Di Matteo hatimaye nafasi yake imechukuliwa na Steve Bruce.

Bruce 55, kwa sasa ndiye aliyechukuwa rasmi dhamana ya kuikwamua Aston Villa ambayo ipo kwenye hali tete ikiwa imepata ushindi mmoja katika mechi 12 ilizocheza.

Bruce anakuwa kocha wa 6 kuingia Villa katika kipindi cha miezi 12 ambapo timu hiyo ilishindwa kufanya vizuri kupitia makocha wote hao.

Kwa upande wa kocha huyo alisema kuwa ameipokea kwa furaha nafasi aliyopewa na timu na kurejea tena kwenye kazi yake kwa mara nyingine.

"Nina nafasi ya pekee kwangu kwa kuwa Villa ni moja ya timu kubwa katika nchi hii." Alisema Bruce.

Comments