Aliyewahi kuwa kocha wa Real Madrid Fabio Capello amesema kuwa kufanya vibaya kwa timu ya Real Madrid kunachangiwa na Mshambuliaji wao nyota Christiano Ronaldo.
Timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha Zinedine Zidane haijapata ushindi katika mechi nne za mwisho dhidi ya Villareal, Las Palmas, Dortmund pamoja na Eibar ambapo katika mechi zote hizo wamepata matokeo ya sare.
Capello alisema Ronaldo ndiye mchezaji tegemeo kwenye timu hiyo hivyo hali ya kukosa ushindi kwa Real Madrid imechangiwa na majeraha yanayomsumbua nyota huyo.
"Ronaldo hajawa fiti kwa asilimia mia tangu alipopatwa na majeraha katika michuano ya UEFA Euro, ni mchezaji bora wakati wote nadhani hii ni sababu pekee Real Madrid kukosa matokeo.
"Tatizo la Real Madrid ni Ronaldo mwenyewe bado hajawa fiti kama ilivyozeleka." Alisema Capello

Comments
Post a Comment