Charlie Nicholas aitoa Man utd nne bora


Mchambuzi wa kituo cha sky sports ametengua msimamo wake wa awali na sasa ameitoa Manchester utd kwenye nne bora kama alivyokuwa amepanga hapo awali.

Charlie amemuingiza Tottenhma hotspurs katika kinyang'anyiro cha ubingwa kutokana na uelekeo mzuri ambao kocha Mauricio Pottechino ameonesha mpaka sasa.

Msambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Celtic amesema kuwa kwa upande wake anadhani kuwa Manchester city, Arsenal, Tottenhma na Liverpool ndizo zitakazoingia nne bora msimu huu.

Akiizungumzia Man utd Nicholas amesema kuwa bado baadhi ya wachezaji wameshindwa kuonesha thamani yao akiwemo Paul Pogba ambaye alisajiliwa kwa dau la paundi 89.5 milioni.

"Kama Pogba angekuwa ametoka moja kwa moja kwenye Academy nadhani mashabiki wasingevumilia, nadhani thamani yake ni kubwa na wanaheshimu hilo ingawa bado hajathibithisha thamani ya paundi 89.5 Milioni." Alisema Nicholas.

Mbali na kiwango kizuri ambacho Liverpool imeonesha hadi sasa lakini Nicholasi ameitoa Liverpool kwenye mbio za ubingwa huku akikisitiza kuwa timu hiyo bado haitoshi kuwa bingwa kutokana na safu mbovu ya ulinzi waliyonayo kulinganisha na timu zingine.


Comments