Timu ya Chelsea jana imevuruga usingizi mnono wa Jose Mourinho baada ya kuichapa Manchester united bao 4-0 katika uwanja wa Stamford Bridge.
Chelsea ilianza kufungua ukurusa wa mabao dakika ya kwanza ya mchezo baada ya Pedro Rodriquez kuwazidi ujanja mabeki wa Manchester united na kutumbukiza mpira wavuni Gary Cahil alifunga bao la pili na kuingoza Chelsea kwenda mapumziko ikiwa na bao 2.
Hali kadhalika mambo hayakuwa mazuri katika kipindi cha pili baada ya Chelsea kuwashinda Manchester united kwa kutumia mashambulizi ya kustukiza ambapo Eden Hazard na N'golo Kante walikamilisha idadi ya goli 4.
Chelsea walionekana kujipanga vema na kutumia vilivyo nafasi walizopata ikiwa ni pamoja na kumpa mwalimu Antonio Konte sifa za kutosha tangu alipoanza kutumia mfumo wa 3-4-3 kwenye mechi tatu za mwisho.
Baada ya ushindi hatimaye Chelsea imerejea tena kwenye nafasi ya tano ikiwa na pointi 19 sawa Tottenham Hotspsurs ikiachwa pointi na Manchester city, Arsenal na Liverpool ambazo zote zina pointi 20.

Comments
Post a Comment