Kocha wa Chelsea amewataka mashabiki wa timu ya hiyo kuwa wavumilivu na matokeo ambayo timu imepata hadi sasa na kuwaahidi kuwa mambo mazuri yanakuja.
Conte ambaye ni kocha wa zamani wa Juventus pamoja na Timu ya taifa ya taifa ya Italy amesema kuwa wanakiwa kumpa muda kwa kuwa kuna mambo mengi hayajakaa sawa kwenye timu hiyo.
Chelsea ambayo msimu ulipoita ilishika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu England imepoteza mechi mfululizo kutoka kwa Liverpoo na Arsenal.
"Hatuna miujiza na kuweza kubadilisha hali tuliyonayo kwa miezi miwili au mitatu, hatuwezi kusahau ya nyuma tulimaliza tukiwa namba 10.
"Unapomaliza kwenye nafai hiyo inamaanisha kuna matatizo, tunatakiwa kubadilisha hali hiyo na kujituma kwa bidii na kwa pamoja tunaweza kufanikisha hili." Alisema Conte

Comments
Post a Comment