Timu ya Paris St Germain (PSG) ya Ufaransa inavutiwa na mpango wa kumsajili mchezaji nyota wa Liverpool Phelipe Coutinho.
Coutinho 24, anazidi kutamba katika ligi ya England tangu aliposajiliwa na Liverpool mwaka 2013 akitokea timu ya Intermilan.
Inasadikika huenda PSG ikatenga dau nono kuishawishi Liverpool kumwachia Countinho ambaye amekuwa akifaanya majukumu mengi ambayo yanainyanyua timu hiyo ikiwemo kufunga magoli na kutoa pasi za mwisho uwanjani.
Hata hivyo habari za ndani kutoka Liverpool zimebainisha kuwa wapo kwenye mchakato wa kumpa mkataba mpya mchezaji huyo ambaye pia ameanza kutolewa macho na Barcelona.

Comments
Post a Comment