De Bruyne kuikosa Manchester Derby kesho


Mshambuliaji wa Manchester city Kevin De Bruyne atakosa mechi ya wapinzani wa jadi kati ya Manchester united na Manchester city hapo kesho kutokana na jeraha la mguu.

Kocha wa Maanchester city Pep Gurdiola amethibisha kuwa De Bruyne ataikosa mechi hiyo kesho hiyo na huenda akacheza mechi ya ligi dhidi ya West Brom.

"De Bruyne hawezi kucheza kesho, ana maumivu kwenye mguu ni matumaini yangu huenda tukawa naye katika  mechi dhidi ya West Brom." Alisema Gurdiola

Mbali na De Bruyne pia beki wa timu hiyo Pablo Zabaleta atakosa mechi hiyo pamoja na hali ya Mashaka kwa Vicent Kompany na Sergio Aguero.

Hata hivyo Gurdiola aliongeza kuwa huenda Kompany na Aguero wakacheza mechi kutoka na uhafadhali wa majeraha yao.

Comments