Gurdiola aonja joto ya jiwe England, city ikifa 2-0 kwa Spurs


Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola kwa mara ya kwanza ameonja joto ya jiwe baada kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Spurs.

Hii ni mechi ya kwanza Gurdiola anapoteza tangu kuanza kwa ligi ya EPL akiwa ameshinda jumla ya mechi 6 na kupoteza mechi ya leo.

Koralov alianza kuipatia Spurs bao la kwanza baada ya kujifunnga wakati akijaribu kuokoa mpira kwenye lango lake huku bao la pili likiwekwa nyavuni na Delle Ali kunako dakika ya 37.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kigumu kwa city baada ya Fernandinho kumfanyia madhambi Son na kusabisha penati lakini hata hivyo Eric Lamela alikosa penati baada ya kipa wa Man city Claudio Bravo kucheza mkwaju huo wa penati.

Mpira uliendelea kuwa wa kushambuliana kwa pande zote mbili hadi pale mwamuzi alipopuliza kipyenga kuhitimisha dakika 90 za mchezo huo.

Comments