Gurdiola azima Internet Mazoezini


Kocha wa Manchester city Pep Gurdiola amefunga huduma ya internet ambayo imefungwa katika uwanja wa mazoezi (WI-FI) wa timu hiyo ili kuwafanya wachezaji kuzingatia mazoezi.

Beki ya Man city Pablo Zabaleta ndiye aliyetoa siri hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo kwa sasa huduma hiyo ya mawasiliano imefungwa rasmi.

"Ni kweli kocha amezuia huduma hiyo, hatuna 3G kwa sasa kocha ametutaka kupata chai na chakula cha mchana pamoja.

"Siku zote nilikuwa na ndoto za kufundishwa na kocha bora maishani mwangu na sasa ndoto yangu imetimia chini ya Gurdiola." Alisema Zabaleta.

Comments