Nyota wa klabu ya Azam FC Hamis Mcha maarufu kama 'Viali' ametamba kuwa kutikisa kwenye ligi kuu ya Vodacom msimu na kuwadhihirishia watanzania ubora wake.
Viali hakupata nafasi ya kufanya mambo makubwa kwenye timu yake Azam kwa kutokana na jeraha la goli ambalo limemsumbua kwa takribani misimu 2 na kumfanya asugue benchi muda.
Mchezaji amefunga mabao 2 hadi katika mechi nne alizocheza ikiwemo mechi dhidi ya Mbeya city na Ruvu Shooting na kutoa pasi 3 za mabao ambazo zimeingoza vema Azam.
"Namshukuru Mungu kwa kunipa afya njema, hatimaye nimerejea tena uwanjani, misimu miwili iliyopita sikufanya vizuri kutokana na majeraha ya goti, lakini sasa nimeanza kurudi kwenye kiwango changu na mashabiki wategemee mambo makubwa.
"Makocha wanafanya mambo makubwa kwenye kikosi chetu, nadhani tuna nafasi ya kujitoa na kufanya mambo makubwa msimu huu," Alisema Mcha.
SOURCE: www.azam.co.tz

Comments
Post a Comment