Kuelekea mechi ya Simba na Yanga leo wafuatao ni wachezaji hatari ambao wanaweza kuwa tishio kwenye lango pinzani na kuyafanya matokeo kuwa kilio kwa upande wa timu zote.
MTN ( Msuva, Tambwe, Ngoma)
Bila shaka hakuna asiyejua uhodari wa mashujaa hawa wa Yanga ambao wamekuwa wasumbufu kwa ngome pinzani na kutengeneza idadi kubwa ya matokeo ikiwemo kupeleka kwa kilio kwa wapinzani wao Simba mara mbili katika mechi za ligi kuu msimu wa 2016/16. Bila shaka Method Mwanjali pamoja na safu yake ya ulinzi akiwemo Novaty Lufunga na Mohamed Hussein wanatakiwa kujipanga vema kukabiliana na tembo hao wa Jangwani.
KIAMA (Kichuya, Ajib, Mavugo)
Ukisikia neno kiama bila shaka lazima uingiwe na hofu, ndivyo ilivyo kwa washambuliaji wa Simba ambao hadi sasa wamefunga zaidi ya goli 7 tangu kuanza kwa msimu. Kichuya aliyetokea Mtibwa amefunga mara nne hadi sasa na kuonesha thamani kwenye timu hiyo akishirikiana vema na Ludit Mavugo mwenye goli tatu pamoja Ibrahim Ajib ambaye amefunga mara mbili hadi sasa. Bila shaka safu ya ulinzi Yanga chini ya Kevin Yondani itakuwa na wakati mgumu kuizuia safu hii ya Simba isilete madhara na kushusha kilio kwa wana Simba.



Comments
Post a Comment