Henderson achukua tuzo ya goli bora mwezi Septemba


Kiungo na Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson ameshinda tuzo ya mfungaji wa goli bora mwezi September zinazotolewa na chama cha soka nchini humo.

Henderson mwenye miaka 26 aliifungia Liverpool bao la pili katika mechi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford baada ya kufunga kwa shuti kali akiwa kwenye umbali mrefu na eneo la goli kipa.

Nahodha huyo wa Liverpool amekuwa na msimu mzuri tangu kuanza kwa ligi ya England na ziku za hivi karibuni alikabidhiwa unahodha England ilipochuana na Slovenia katika hatua za kusaka tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Urusi mwaka 2018.


Comments