Herrera aitwa timu ya taifa


Kiungo wa Manchester united Ander Herrera kwa mara ya ameitwa kwenye timu ya taifa Spain baada ya kuonesha kiwango tangu alipopewa nafasi na kocha wa Manchester united Jose Mourinho.

Herrera 27, ataungana na kikosi cha Julin Lopetegui siku ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Italy na Albania ikiwa ni mwendelezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Russia.

Kiungo huyo alipewa sifa kedekede na Mourinho kutokana na kiwango bora alichoonesha tangu alipochukua nafasi ya Mouraine Fellain ambaye ameshindwa kumtumia Paul Pogba vema kunako uwanja.

"Herrera ni mchezaji bora kwetu kwa sasa anamfanya Pogba kucheza katika nafasi tofauti na kutengeneza nafasi za magoli," Alisema Mourinho.

Comments