John Terry arudi kamili kuivaa Man Utd Jumapili


Beki na nahodha wa Chelsea John Terry amerejea uwanjani baada ya kupona majeraha ya goti na atakuwa fiti kuivaa Manchester united katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya jumapili.

Terry mwenye umri wa miaka 35 alishiriki mechi ya mwisho wakati Chelsea ilipotoka sare ya bao 1-1 na Swannsea Septemba 11 mwaka huu.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa beki huyo yuko fiti na huenda akacheza mechi ya jumapili dhidi ya Chelsea.

"John Terry anaendelea vizuri, amepona majeraha yake na ameanza mazoezi na timu na atakuwa tayari kwa ajili ya mechi." Alisema Conte

Comments