Juma Mwambusi kuliongoza jahazi la Yanga na JKT Ruvu


Baada ya kujiuzulu kwa kocha mkuu Hans Van der Pluijm kocha msaidizi wa timu hiyo Juma Mwambusi ndiye atakayeiongoza Yanga mechi ya kipolo cha ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa huenda kocha akatimkia Prisons tangu  kuwasili kwa George Lwandamina ambaye ndiye mrithi Pluijm.

Hata hivyo Mwambusi amekanusha taarifa za kujiuzulu Yanga na kusisitiza kuwa hana mpango wa kumtika klabuni hapo na kutua Prisons.

"Jitihada zangu ni kuiongoza Yanga ipate matokeo mazuri, na tumejiandaa vizuri na mazoezi kupambana na JKT Ruvu leo.

"Taarifa ya kwamba ninataka kujiuzulu na kutimkia prisons hazina ukweli wowote, na wala sina mpango kutua prisons." Alisema Mwambusi.

Comments