Timu ya Juventus inataka kumtumia beki wao kitasa Leonardo Bonucci kama sehemu ya kumnasa kiungo wa Chelsea Cesc Fabrigas.
Fabrigas ameanza kuwa na maisha magumu ya kupata namba kwenye kikosi cha kwanza tangu kutua kwa kocha Antonio Conte ambaye hana imani ya kumtumia Fabrigas kwenye mfumo wake.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte hana imani na safu ya ulinzi ya chelsea baada ya kuanza kupoteza matumaini na Gary Cahil ambaye aliigharimu Chelsea katika mechi dhidi ya Swansea na Arsenal.
Huenda Juvuntes ikafanikiwa kukamilisha zoezi hilo la kumnasa kiungo huyo kwa kuwa Conte ana muhitaji Bonucci ambaye ni beki wake wa zamani kwa udi na uvumba.

Comments
Post a Comment