Kocha aliyerejea Majimaji kwa mara nyingine Kalimangonga Ongala 'Kally' kwa mara ya kwanza ameipa Majimaji pointi 3 tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.
Majimaji leo kwenye uwanja wa nyambani imeweza kuibuka na ushindi bao 1-0 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza baada ya kupoteza mechi 6 za mwanzo.
Kally ambaye msimu uliopita alikabidhiwa timu hiyo na kuinusuru Majimaji isishuke daraja amerejea tena kwa kishindo baada ya kuleta ushindi wa kwanza kwenye timu hiyo muda baada ya kurejea Majimaji.
Kwa mara ya kwanza majimaji imesimama kwa pointi 3 kwenye msimamo wa ligi kuu, tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi ya Vodacom 2016/17.

Comments
Post a Comment