Kally Ongala na Majimaji FC damu damu, apata ushindi wa kwanza ugenini.


Timu ya Majimaji jana ikiwa ugenini iliweza katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani wa Mwanza iliweza kupata ushindi wa pili baada ya kuifunga Toto Africans bao 2-1.

Majimaji imepata ushindi wa kwanza ugenini ikiwa  ni siku chache tangu kutua kwa Kally Ongala kwenye timu hiyo na kuweza kupata ushindi wake kwanza dhidi ya Mbao FC katika uwanja wa Majimaji Songea.

Kally, ambaye amewahi kuwa kwenye benchi la ufundi Azam FC ameonesha uzoefu wake katika kikosi cha Majimaji baada ya kupatiwa nafasi ya kuindoa timu hiyo kwenye ramani mbovu hii ikiwa ni mara ya pili.

Licha ya Toto Africans kuanza kupata bao la kuongoza kwenye mechi hiyo lakini Majimaji iliweza kuchomoa bao hilo na kupata lingine la ushindi.

Kally Ongala amefanikiwa kukusanya jumla ya pointi 6 katika mechi nne tangu alipoichukua Majimaji mwezi Septemba mwaka huu.

Comments