Kila la kheri Serengeti boys dhidi ya Congo Brazzaville


Timu ya Serengeti boys leo itaamua hatma yake kufuzu kuelekea fainali na kombe la mataifa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika mwakani endapo itaindoa Congo Brazzaville kwenye mechi ya marudiano.

Awali timu hiyo ya Vijana ilitoka na ushindi wa mabao 3-2 katika uwanja wa taifa walipowakaribisha vijana wenzao kutoka Congo katika mechi ya kwanza.

Bado Serengeti boys ina kibarua kizito cha kutafuta sare au ushindi ili kujihakikishia tiketi ya kushiriki michuano hiyo hapo mwakani.

Binafsi, tunaitakia Kila kheri Serengeti boys ili ikapate nafasi ya kuipeperusha vema bendera ya tanzania kwenye medani ya soka baada ya kupata mazuri ya kushiriki fainali hizo mwaka 2017.

Comments