Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa ana ndoto ya kuachana na maisha ya soka hapo baadae akiwa na timu hiyo pekee.
Klopp 49 amesema anategemea kustaafu masuala ya mpira katika kipindi cha miaka 10 ijayo kutoka sasa akiwa na mipango ya kufundisha timu ya Liverpool mpaka atakapoamua kutandika daluga.
"Nataka niachane na soka nikifika miaka 60, nitakuwa nimefundisha timu tatu ambazo ni nzuri duniani yaani Mainz, Dortmund na Liverpool nadhani ni timu bora kwenye maisha yangu."
"Nadhani katika kipindi cha miaka 60 itakuwa inatosha sasa, kufundisha timu 3 bora ni jambo linalopendeza" Alisema Klopp
Pia kocha huyo amekisifu kikosi chake ambacho kimeendelea kufanya vizuri katika ligi hadi sasa na kupata wastani wa matokeo mazuri katika mechi walizocheza.
"Kikosi ni bora na kinafanya vizuri kwa sasa nina imani na timu yangu nadhani mechi dhidi ya Swansea tuna tumaini la kushinda na kupata pointi 3." Aliongeza Klopp

Comments
Post a Comment