Baada ya kocha Rogasian Kaijage kuachia ngazi kuinoa Toto African kocha wa sasa aliyekabidhiwa mikoba ya Kaijage, Khalifan Ngasa amesema kuwa timu hiyo ilikosa umoja.
Akizungumza wakati akiwa mazoezini na Timu hiyo Khalifan Ngassa alisema kuwa Toto African ni timu nzuri isipokuwa kulikuwa hakuna maelewano mazuri kati ya walimu na wachezaji hali iliyopelekea na wachezaji kukosa umoja.
"Nimezungumza nao nimegundua hapakuwa na maelewano mazuri baina ya wachezaji na kocha, vilevile wachezaji walikosa maelewano nadhani kila kitu kitakuwa sawa." Alisema Ngassa
Pia kocha huyo ambaye kwa mara ya kwanza ataingia kibaruani kuchuana na Kagera Sugar katika uwanja wa kaitaba amesema kuwa hana wasi na mchezo huo ana imani Toto itafanya vizuri.
"Mechi ya leo ni kama mechi nyingine bila shaka sioni tatizo kwa upande wangu, nategemea mambo mazuri kwa vijana wangu." Aliongeza kocha huyo
Comments
Post a Comment