Ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Novemba mosi mwaka huu ambapo timu 12 zitashiriki ligi hiyo.
Zoezi la ukaguzi wa fomu za usajili utaanza kesho Octoba 8 hadi 10 mwaka huu na majina ya usajili yatatangazwa pamoja na kutumwa majina kwa klabu shiriki kwa njia ya barua pepe.
Pamoja na zoezi la usajili pia uongozi umetoa nafasi ya kutoa pingamizi Octoba 11 hadi 12 ambapo Octoba 15 ni siku ya kusikiliza pingamizi na majina hayo yatatangazwa kabla ya Octoba 20 ya mwaka huu.
Pia kabla ya kuanza kwa ligi hiyo kutakuwa na utaratibu wa kuwasilisha rangi za jezi zitakazotumika nyumbani na ugenini huku timu zote zikitakiwa kusafiri na jezi zote mbili ili kuepusha mwingiliano wa Rangi.
Ligi hiyo itahusisha jopo la makocha watakaokuwa wakichagua wachezaji nyota watakaounda timu ya taifa ambao watagharamiwa na TFF.

Comments
Post a Comment