Ligi ya wanawake kurushwa live Azam TV.


Baada ya ligi ya Vodacom kushika kasi kutokana na udhamini wa kituo cha Azam kurusha matangazo hayo pia kituo hicho kitarusha 'live' ligi ya soka ya wanawake inayotarajiwa kuanza Novemba 1 mwaka huu.

Ligi hiyo imegawanywa kwenye makundi mawili ambapo kundi A lina timu za Viva Queens ya Mtwara, Fair Play ya Tanga, Mlandizi Queens ya Pwani pamoja na Mburahati Queens, Evergreen Queens na JKT Queens za Dar es Salaam wakati kundi B zimo Marsh Academy ya Mwanza, Baobab Queens ya Dodoma, Majengo Women ya Singida, Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queens ya Kagera na Panama FC ya Iringa.
Mzungo wa ligi hiyo utachakua takribani wiki 3 hadi Novemba 20 mwaka huu ambapo mzunguko wa pili utaanza January 4 hadi February mosi mwakani.

Comments