Liverpool yaendelea kufanya yake Epl, yaichapa 2-1 West Brom


Timu ya Liverpool jana ikiwa katika uwanja wa Anfield ilitoka na pointi 3 za ushindi baada ya kuichapa West Brom 2-1.

Mabao ya Liverpool yalifungwa kipindi cha kwanza na Sadio Mane pamoja na Phelipe Coutinho.

Liverpool imeendelea kuwa bora msimu huu kutoka na soka lao lenye kasi uwanjani uwanjani ikiwa ndiyo timu pekee ambayo imekimbia zaidi uwanjani katika ligi ya EPL.

Ushindi huo umeingoza Liverpool yenye pointing 20 juu ya msimamo wa ligi kuu ikisubiri matokeo ya mechi za leo.

Comments