Majimaji ya Kally yaitegea pua Azam


Ananyedhani Timu ya Azam iko pazuri kuliko Majimaji anajidanganya baada ya Kally kudhihirisha hilo akichomoka na ushindi wa 3 dhidi ya African Lyon katika uwanja wa taifa.

Majimaji ya Songea imeendelea kuchomoka usingizini taratibu tangu Kalimangonga Ongala arejee kuwa mwalimu kwa mara kwenye timu hiyo.

Hadi sasa Azam inaiacha Majimaji kwa pointi 4 licha ya kupoteza idadi ya mechi sita tangu kuanza kwa ligi ya Vodacom na huenda Majimaji ikaendelea kunasa harufu ya Azam endapo timu hiyo itaendelea kufanya makubwa uwanjani.

Azam bado haichezi katika kiwango chake kama ilivyokuwa katika misimu mingine iliyopita, hadi sasa imekusanya jumla ya pointi 13 ikiwa ni pamoja na kufanya  vibaya katika michezo ya mwisho.

Majimaji ameanza kujinasua mkiani baada ya kupiga chini Toto Africans ambayo ina pointi 8 hadi sasa na Majimaji ikiwa na pointi 9.

Timu hiyo imeanza kurejea kwenye hali ya ushindi tangu kutua kwa Kalimangonga Ongala ambaye msimu uliopita aliichukua Majimaji katika dakika za majeruhi na kuinusuru timu hiyo isichungulie ligi daraja la kwanza.




Comments