Timu ya Afrika Kusini Mamelody Sundown imefanikiwa kutwaa taji la klabu bingwa Afrika baada ya kuishinda Zamaleki ya Misri.
Licha ya kufungwa bao 1-0 na Zamaleck kwenye mchezo wa jana lakini bao hilo halikutosha kuwanyima ushindi Mamelody Sundown ambao walishinda bao 3-0 nyumbani.
Timu hiyo itapata fursa ya kushiriki fainali za kuitafuta klabu iliyo bora zaidi duniani, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa FIFA kuwashindanisha mabingwa kutoka mabara mbali mbali duniani.

Comments
Post a Comment