Manara apigwa faini na TFF


Mkurugenzi wa kitengo cha habari na mawasiliano wa timu ya Simba Haji Manara amepigwa faini ya Tsh. 200,000.

Kamati ya bodi ya ligi ya uendeshaji na usimamizi iliamua kumtwanga Haji Manara faini hiyo kutokana na kitendo chake cha kuzama uwanjani kinyume na utaratibu.

Manara aliingia uwanjani katika mechi dhidi ya watani wao jadi Yanga kuwatuliza mashabiki wa Simba waliokuwa waking'oa viti jambo ambalo hakutakiwa kufanya.

Kamati hiyo ilitumia kipengele cha kipengele cha kanuni ya 14(10) kumbana Haji Manara na kuwajibika na ulipaji wa faini hiyo.

Comments