Manchester city yakabwa koo na Everton, zatoka 1-1 Etihad.


Kocha wa Manchester Pep Gurdiola bado anaendelea kukaribishwa EPL baada ya kukubali kutoka sare ya bao 1-1 na Everton.

Everton walianza kupata bao la kuongoza kupitia Romeu Lukaku aliyefunga dakika ya 64 na lile la Manchester city lilifungwa na Nolito dakika ya 72.

Pamoja na Manchester city kuliandama lango la Everton kwa muda mwingi lakini bado Everton ilionekana kuwa imara katika safu ya ulinzi.

Katika Mechi hiyo Manchester city ilitengeneza nafasi nyingi ikiwemo penati mbili ambazo Kevin De Bruyne pamoja Sergio Aguero walikosa.

Mpaka mwisho wa mchezo kiungo David Silva ndiye aliyetangazwa kuwa nyota wa mchezo huo kutokana kiwango bora alichokionesha pamoja na kutengeneza nafasi nyingi.

Comments