Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeutaka uongozi wa Yanga kutoa ufafanuzi kwa kile kinachoripotiwa kuhusu bodi ya wadhamini kuingia makataba wa kuikodisha kwa kampuni inayofahamika kwa jina la Yanga Yetu.
TFF imesema kuwa haipingi mabadiliko katika timu ya Yanga isipokuwa inataka kujua taratibu na sheria za mfumo huo kama zimefuatwa kama inayotakiwa.
" Msimamo wa TFF ni kuwa timu ya Yanga ipo kama ilivyokuwa kwa mujibu wa taratibu za TFF,CAF na FIFA hadi tutakapopata barua kutoka Yanga na wanatambua uongozi mwenyekiti Yusuph Manji pamoja na katibu Baraka Deusdedith." alisema Celestine Mwesigwa ambaye ni katibu wa TFF
Mwesigwa alisema kuwa wanataka kuona kilichopo kwenye mkataba kabla ya kushauri uongozi ili kuangalia kama vinakwenda sambamba na matwaka ya CAF pamoja na FIFA ili kuondoa malalamiko yanayofika kwenye Shirikisho hilo kwani wapo wengine wamekuwa wakiomba idhini TFF hata kwenda kuwaona viongoz wa Serikali.
Aidha katibu huyo wa TFF aliongeza kuwa bado wataendelea kuwasiliana na Viongozi wa Yanga wanaofahamika akiwemo mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji pamoja na katibu Deusdedit na siyo bodi ya wadhamini wa timu hiyo.

Comments
Post a Comment