Mwamuzi aliyeamua mechi ya Simba na Yanga Martin Saanya amefungiwa miaka 2 pamoja na msaidizi wake namba 1 Samuel Mpenzu baada ya bodi ya shriikisho la soka Tanzania kufikia maamuzi hayo.
Mwamuzi alikuwa chanzo cha vurugu kwenye mechi hiyo iliyopigwa Octoba 1 mwaka huu kutokana na maamuzi ya yenye utata hali ambayo ilichangia kusimama kwa mechi kwa takribani dakika 9 kutokana na vujo za mashabiki pamoja na kukosa maelewano dhidi ya wachezaji wa Simba.
Kwa upande mwingine pia bodi hiyo imefuta kadi nyekundu ya nahodha wa Simba Jonas Mkude baada ya kugundua kuwa hakuwa na makosa kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa.
Hivi karibuni kocha wa Mwadui Jamhuri Kihwelo alitangaza kujiuzulu kufundisha soka Tanzania kutokana na ukosefu kwa kutenda haki kwa waamuzi ambapo kulingana na Julio alidai wamuuzi wanamrudisha nyuma kwenye ligi.
Hata hivyo vurugu katika mechi hiyo zimeigharimu Simba na Yanga baada ya serikali kuwafungia kutumia uwanja wa taifa kwa muda usiojulikana.
Comments
Post a Comment