Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo amekiri kuwa mambo ni magumu katika ligi ya Vodacom na kuwataka mashabiki wa Simba wampe muda.
Mavugo ambaye amewahi kujibebea umaarufu mkubwa Afrika ya Mashariki akiwa na Vital O' ya Burundi amesema moja ya mazingira yanayompa wakati mgumu ni viwanja vibovu vya Tanzania.
"Mambo bado ni magumu naomba mnipe muda wa kuzoea zaidi mazingira, unajua kuna viwanja ni vibovu hapa Tanzania si kama kule kwetu Burundi.
"Burundi hakuna viwanja vibovu kama ilivyo Tanzania ndiyo maana nilikuwa nafunga sana, mashabiki naombeni mnipe muda." Alisema Mavugo
Laudit Mavugo amefunga jumla ya magoli 4 hadi sasa katika mechi 11 alizocheza tangu alipojiunga na Simba akiachwa goli 4 na Shiza Kichuya ambaye amechungulia nyavu mara 8 hadi sasa.
Comments
Post a Comment