Mbeya city yatamba kuigalagaza Simba kama kawa


Timu ya Mbeya city wameionya timu Simba kuwa haitapata ushindi katika mechi ya ligi kuu itakayochezwa katika uwanja wa sokoine hapo kesho.

Mbeya city kupitia msemaji wao Dismas Ten amesema kuwa wataendelea kuiburuza timu ya Simba kama ilivyo kawaida yao tangu walivyopanda daraja chini ya kocha Juma Mwambusi.

"Historia yetu kwa Simba inafahamika nadhani tutapata ushindi kama ilivyokawaida, tutatoka na pointi hivyo Simba isitegemee kupata pointi 3 Sokoine." Alisema Ten

Mbali na mechi hiyo ya Simba pia timu ya Yanga itakipiga na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru hapo kesho ambapo Azam itaikabiri Stand Utd katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.

Comments