Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea leo ambapo kutakuwa na mechi mbili ambazo zinachezwa katika viwanja tofauti ukiwemo mchezo kati ya Mbeya City na Stand United ya Shinyanga katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Pia vijana wa Mecky Mexime, Kagera Sugar katika uwanja wa kaitaba wanaikaribisha Toto Africans ambayo leo itaingia uwanjani ikiwa na kocha mpya Khalifan Ngassa baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Rogasian Kaijage kuachia ngazi.
Mbali na michezo ya leo pia kesho jumamosi Majimaji chini ya kocha Kali Ongala itakuwa kibaruani kutafuta ushindi wake wa kwanza dhidi ya Mbao FC ya Mwanza na JKT Ruvu wataikaribisha Ndanda FC katika uwanja wa mabatini.

Comments
Post a Comment