Mechi tatu kunogesha ligi kuu ya Vodacom leo.


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara leo itaendelea kutimua vumbi ambapo michezo mitatu itachezwa kwenye viwanja tofauti.

Timu ya Simba itaikaribisha timu ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa uhuru ambapo leo majira ya saa 10 za jioni mechi hiyo itakuwa inachezwa na mwamuzi wa mchezo ni Hussein Athumani kutoka Katavi akisaidiwa Joseph Bulali kutoka Tanga pamoja na Sylvester Mwanga kutoka Kilimanjaro.

Mechi nyingine ni kati ya JKT Ruvu na Mwadui FC ya Shinyanga ambayo itachezwa katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, pia Stand united itamenyamana na African Lyon katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.


Comments