Mourinho: Rooney haendi kokote


Licha ya kuvuma kwa taarifa za kutimka kwa mshambuliaji wa Manchester united Wayne Rooney kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ameibuka na kusema nahodha huyo hataondoka kwenye timu hiyo.

Kumekuwa na taarifa kuwa huenda Wayne Rooney akatimka katika Manchester united na kutua LA Galaxy ya Marekani au kutua kwenye moja ya klabu zinazotamba nchini China.

Rooney mwenye miaka 31 ameanza kupoteza furaha yake ya awali baada ya kuanza kusugua benchi katika mechi kadhaa ambazo timu hiyo imecheza mpaka sasa.

"Hakuna ukwel katika hilo, ingawa ana miaka 31 moja lakini ninajua ana uwezo mkubwa wa kucheza uwanjani tena kwa kiwango cha juu.

"Ninachoweza kusema ni kuwa Rooney ni mchezaji wetu muhimu, mwenye kiwango bora na hataondoka United." Alisema Mourinho.

Comments