Mzamiru, Mavugo waing'arisha Simba taifa


Timu ya Simba imeendeleza ubabe baada ya ligi kuu baada ya kuichapa Toto Africans bao 3-0.

Kiungo wa Simba Mzamiru Yasin ameendelea kuwa na wakati mzuri mwezi baada ya kuifungia Simba mabao 2 hapo jana na bao la tatu lilifungwa na Laudit Mavugo.

Katika mechi hiyo Simba ilionekana kuwamudu Toto Africans katika eneo la kati kati na kuipa wakati mgumu timu hiyo kwa dakika zote 90.

Ushindi unaiongoza Simba  juu ya msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 29 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 21 pamoja na Stand united.

Comments