Nani kuibuka mbabe Mourinho vs Gurdiola leo.


Baada ya Jose Mourinho kuchezea kipigo cha bao 2- 1 katika mechi ya ligi waliyokutana hatimaye mafahali hao wanakutana tena leo kwenye dimba la Old Trafford.

Kuna nafasi ya timu moja pekee kutinga kwenye hatua ya robo fainali siku ya leo endapo yeyote atafanikiwa kuondoka na ushindi.

Katika rekodi ya ushindi ni wazi kuwa Gurdiola amemfunga mara nyingi Mourinho kuliko Mourinho alivyofanya hivyo kwa Gurdiola.

Wakati Mourinho alipotua La liga kuinoa Real Madrid, Gurdiola ndiye aliyekuwa kocha wa Barcelona, kwa pamoja wamefanikiwa kukutana mara 12 ambapo Gurdiola alimfunga Mourinho mara 5, na Mourinho akifanya hivyo mara 2, pamoja na sare 4.

Mourinho amewahi pia kumfunga Pep Gurdiola wakati huo akiwa na Intermilan mwaka 2010, na kumwondoa Barcelona mashindanoni baada ya kumfunga bao 3-1 nyumbani na Barcelona ilipata ushindi wa bao 1 pekee katika uwanja wa Camp Nou.

Makocha hao wamekutana tena katika jiji la Manchester ambapo kuna uhasimu mkubwa kati ya Manchester united na Manchester city ambapo katika mechi ya kwanza Gurdiola amefanikiwa kumfunga Jose Mourinho.

Hii ni nafasi ya pekee kwa Jose Mourinho kulipa kisasi kwa Gurdiola kwa mara nyingine anabahatika tena kuwa katika uwanja wa nyumbani ambapo mara ya mwisho alipoteza kwa kufungwa bao 2-1 na Gurdiola.

Ipo haja ya kusubiri mechi hiyo ili kufahamu nani ataibuka mbabe dhidi ya mwenzie katika mchezo utaokaapigwa majira ya saa nne kasarobo kwa saa za Afrika ya Mashariki.


Comments