Beki wa Real Madrid Sergio Ramos atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kupata majeraha ya goti.
Ramos aliumia wakati Hispania ikichuana na Albania katika mechi ambayo timu hiyo ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao magoli 2-0.
Nguli huyo wa Real Madrid atakosa michezo minne ya la Liga ukiwemo ule wa Real Betis, Athletic Bilbao, Alaves na Leganes pamoja na michezo miwili ya klabu bingwa Ulaya..
Sergio Ramos 30, atarejea tena uwanja November 20 katika mechi dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid.

Comments
Post a Comment