Rasmi Yanga ni mali ya Manji kwa miaka 10.


Timu ya Yanga kupitia kupitia baraza lake la wadhamini imekabidhi rasmi timu kwa kampuni ya Yanga yetu inayomilikiwa na mwenyekiti wake Yusuph Manji,

Wakati Simba ikiwa haijakamilisha mchakato wao wa kukabidhi timu yao kwa Mohamed Dewji 'MO' taarifa za ndani kutoka katika timu ya Yanga zimethibitisha mchakato huo umekamilika rasmi.

Hivi karibuni mwenyekiti huyo alikabidhi eneo la hekari zisizopungua 700 katika eneo la gezaulole maeneo ya kigambo linalopokana na ufukwe wa bahari maalum kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa timu hiyo, na shughuli zingine za kukuza uchumi wa Yanga.




Comments