Serengeti Boys yang'olewa na Congo Brazzaville


Kwa kile ambacho kilisemwa awali kuhusiana na Serengeti boys kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Madgascar kilikuwa si sahihi bali vijana hao wameondolewa kwenye fainali hizo baada ya kufungwa bao 1-0.

Taarifa Rasmi kutoka TFF zimethibitisha kuwa Serengeti Boys ilikubali kichapo katika dakika za nyongeza ambapo Congo Brazaville walipata ushindi bao hilo kunako na dakika ya 92 kabla ya kumalizika kwa mpira.

Kwa matokeo hayo ni wazi kuwa Serengeti boys hawajafuzu fainali hizo kama ambavyo taarifa zilithibitisha hapo awali.

Comments