Mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
Kichuya amebeba tuzo hiyo baada ya kuwapiku Adam Kingwande wa Stand united pamoja na Omary Mponda wa Ndanda FC.
Nyota huyo ambaye ameshika umaarufu katika timu ya Simba amefunga jumla ya magoli saba katika mechi 9 alizocheza hadi sasa na kuongoza katika orodha ya wafungaji mabao kwenye ligi kuu ya Vodacom.
Kichuya atazawadiwa kiasi cha shilingi ,1000,000 za kitanzania kama zawadi na mdhamini wa ligi hiyo ambao ni kampuni ya Vodacom.

Comments
Post a Comment