Shiza kichuya ndiye habari ya mjini kwa mashabiki wa Simba.


Mchezaji wa Simba Shiza Kichuya amekuwa gumzo kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na kazi nzuri anayoifanya uwanjani tangu aliposajiliwa akitokea Mtibwa Sugar.

Shiza ameifungia Simba mabao 6 hadi sasa na kuwafunika baadhi ya washambuliaji wa ndani na wa kigeni akiwemo Amis Tambwe, Donald Ngoma, Laudit Mavugo, John Bocco pamoja na Fredrick Blagnon.

Baadhi mashabiki wa Simba wamesema kuwa wanajivunia Shiza Kichuya kutokana na jitihada kubwa anazozifanya na kile kinachodaiwa kuwa amezidi kudhihirisha thamani yake ndani ya klabu Simba.

"Kichuya ni mchezaji bora kwenye timu ya Simba, anaonesha jitihada zake na pia ni mchezaji anayejituma ni moja kati ya washambuliaji hatari kwenye ligi hadi sasa." Anasema Jumanne ambaye ni mshabiki wa Simba

"Kwa upande wangu naona tumepata Shujaa, tangu alipoondoka Emmanuel Okwi nadhani sasa tumeanza kupata mrithi wake kwenye timu." Aliongeza shabiki huyo.


Comments