Simba walivyoikata kauli Mbeya City


Licha ya Mbeya city kutamba kuiangusha Simba katika uwanja wa Sokoine lakini imeshindwa kufanya hivyo baada ya kukubali kipigo cha bao 2-0.

Awali Mbeya city walijinadi kupitia rekodi yao dhidi ya Simba lakini hadi kufikia jana Simba ilikuwa imepata ushindi wa pili dhidi ya timu hiyo.

Simba walipata mabao ya ushindi kupitia Ibrahimu Ajib Migomba aliyefunga kwa mpira wa adhabu ndogo na Shiza kichuya alityefunga safari ya ushindi wa Simba baada ya kufunga bao la pili katika dakika ya 34.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikifuatiwa na Stand united zote kwa pamoja zikiwa hazijapoteza mechi yoyote hadi sasa.

Comments